Vuguvugu la Uarabuni

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
       Serikali imeondolewa madarakani       Vurumai endelevu za raia wanaodai mabadiliko ya kiserikali       Maandamano na hatimaye mabadiliko ya kiserikali
      Maandamano makubwa kabisa       Maandamano madogo       Maandamano nje ya ulimwengu wa Kiarabu

Vuguvugu la Uarabuni au Vuguvuru la Kiarabu, Mchipuko wa Uarabuni (Kiarabu: الربيع العربي ‎, kutoka kiing. Arab Spring) ni istilahi iliyokuwa inatumika na vyombo vya habari kwa ajili ya wimbi la mapinduzi la migomo na maandamano yasiyo-na-fujo na yenye-fujo, vurumai, machafuko na vita ya yenyewe kwa wenyewe iliyoanza mnamo tarehe 18 Desemba 2010 katika nchi za Kiarabu.[1]

Watawala waliolazimika kutoka madarakani huko nchini Tunisia, Misri (mara mbili), Libya na Yemen. Machafuko ya kiraia yalitokea huko nchini Bahrain na Syria. Maandamano makubwa katika historia yalitokea huko nchini Algeria, Iraq, Jordan, Kuwait, Morocco na Sudan. Maandamano madogo yalitokea huko nchini Mauritania, Omani, Saudia, Jibuti, Sahara ya Magharibi na Palestina. Kulikuwa na maandamano kiasi kutoka katika nchi ambazo sio sehemu ya Ulimwengu wa Waarabu kama vile Uajemi na Israel.

Kulikuwa na mikinzano huko mipakani mwa nchi ya Israel, na maandamano ya Wakhuzestan wachache wa Kiarabu uliyotokea mwaka 2011. Huko Mali, wapiganaji wa Kituareg wakati wanarudi kutoka katika vita ya wenyewe kwa wenyewe ya Libya walichochea mzozo uliotafsiriwa kama sehemu ya "Vuguvugu la Kiarabu"" kwa upande wa nchi za Afrika Kaskazini. Mikinzano ya vikundi vya kimadhehebu iliyotokea huko Lebanoni ilionekana kuchochewa na machafuko ya Syria hivyo basi imechukuliwa kama Vuguvugu la Kiarabu.

Maandamano haya yaliambatana na kampeni za kupinga mambo mbalimbali, migomo, mashambulizi, matembezi ya miguu kwa masafa marefu, vilevile matumizi ya mitandao ya kijamiii kwa kuhamasisha na kuongeza ufahamikaji wa suala lenyewe katika jamii husika katika ulimwengu wa intaneti..

Vuguvugu nyingi za Kiarabu ziliambatana na fujo za kila aina hasa kwa kufuatia mamlaka kutaka kuzuia harakati hizi. Kwa maana hiyo, waandamanaji nao hawakubali kurudi nyuma katika suala zima la kupigania hicho walichokuwa wanakiamini. Msemo mkubwa uliokuwa unatumiwa na wagomaji katika ulimwengu wa Kiarabu ulikuwa Ash-sha`b yurid isqat an-nizam ("watu wanataka kuuangusha utawala wa kidhalimu").[2][3]

Baadhi ya watafiti wamelifananisha suala hili kama zile vuguvugu za mapinduzi yaliyotokea mwaka 1989 huko Ulaya ya Mashariki au Mapinduzi ya 1848 katika majimbo ya Ujerumani.

Kuanza kwa vuguvugu[hariri | hariri chanzo]

Mfululizo wa migomo na maandamano katika Mashariki ya Kati na Afrika Kaskazini, ulianzia nchini Tunisia mnamo tarehe 18 Desemba 2010 kwa kufuatia Mohamed Bouazizi kujilipua na mafuta ya taa kwa kupinga manyanyaso na rushwa kutoka kwa maafisa wa polisi. Maandamano haya yaliamsha fujo nyengine nje ya mji ambao tukio hili limetokea na kupelekea fujo na maandamano katika nchi mbalimbali za Kiarabu.

Matukio[hariri | hariri chanzo]

Safu hii inaonesha baadhi ya mifululizo ya matukio yaliyotokana na vuguvugu la kwanza la Tunisia kisha kuhamia nchi nyingine za Uarabuni.

  • Desemba 18, 2010: Bendera ya Tunisia Tunisia, maandamano yanaanza, baada ya Mohammed kujilipua na moto.
  • Desemba 29, 2010: Bendera ya Algeria Algeria, maandamano yanaanza.
  • Januari 13 16, 2011: Bendera ya Libya Libya, waandamanaji walidhibitiwa.
  • Januari 14, 2011: Bendera ya Jordan Jordan, maandamano yanaanza.
  • Januari 14, 2011: Bendera ya Tunisia Tunisia, serikali imeanguka.
  • Januari 17, 2011: Bendera ya Omani Oman maandamano madogo yalianza.
  • Januari 18, 2011: Bendera ya Yemen Yemen, maandamano yanaanza.
  • Januari 25, 2011: Bendera ya Misri Egypt, maandamano yanaanza.
  • Januari 26, 2011: Bendera ya Syria Syria, mtu mmoja kajitia moto.
  • Januari 28, 2011: Bendera ya Palestinian territories Palestine, maandamano yanaanza.
  • Januari 28, 2011: Bendera ya Jibuti Djibouti maandamano madogo yalianza.
  • Januari 30, 2011: Bendera ya Sudan Sudan, maandamano yanaanza.
  • Februari 1, 2011: Bendera ya Jordan Jordan, serikali imeondolewa.
  • Februari 10, 2011: Bendera ya Misri Egypt, Rais, na makamu wake wamekabidhi madaraka.
  • Februari 10, 2011: Bendera ya Iraq Iraq maandamano madogo yalipangwa. Nouri al-Maliki anatangaza ya kwamba uchaguzi ujao hatogombea.
  • Februari 11, 2011: Bendera ya Misri Egypt, Rais Hosni Mubarak anajiuzuru.
  • Februari 14, 2011: Bendera ya Bahrain Bahrain, maandamano yanaanza.
  • Februari 15, 2011: Bendera ya Libya Libya kivumbi cha maanadamano kinaanza tena.
  • Februari 19, 2011: Bendera ya Kuwait Kuwait, maandamano yanaanza.
  • Februari 20, 2011: Bendera ya Moroko Morocco, maandamano yanaanza.
  • Februari 25, 2011: Bendera ya Mauritania Mauritania, maandamano yanaanza.
  • Februari 27, 2011: Bendera ya Lebanon Lebanon, maandamano yanaanza.
  • Machi 2011: Bendera ya Jibuti Djibouti, maandamano yanaisha.
  • Machi 3, 2011: Bendera ya Libya Libya kiongozi Muammar Gaddafi anapoteza nguvu ya kuingoza Libya.
  • MachI 5, 2011: Bendera ya Libya Libya Kikosi cha Anga cha Libya chaanza kulipua miji mikubwa. Upinzani ukalazimika kusanda.
  • Machi 11, 2011: Bendera ya Saudi Arabia Saudi Arabia, maandamano yanaanza.
  • Machi 15, 2011: Bendera ya Syria Syria, maandamano yanaanza.
  • March 19, 2011: Bendera ya Libya Libya, bombing by foreign air forces began.
  • Aprili 15, 2011: Bendera ya Uajemi Iran, maandamano yanaanza.
  • Aprili 18, 2011: Bendera ya Uajemi Iran, maandamano yanaisha.
  • Mei 2011: Bendera ya Omani Oman, maandamano yanaisha.
  • Mei 15, 2011: Bendera ya Israel Israel, maandamano yanaanza.
  • Juni 5, 2011: Bendera ya Israel Israel, maandamano yanaisha.
  • Agosti 3, 2011: Bendera ya Misri Egypt, Kesi ya Hosni Mubarak inaanza.
  • Agosti 21-22, 2011: Bendera ya Libya Libya Wapinzani nao wameingia mji mkuu Tripoli.
  • Septemba 29, 2011: Bendera ya Saudi Arabia Saudi Arabia, chaguzi zilifanyika.
  • Oktoba 20, 2011: Bendera ya Libya Libya mji wa Sirte, Muammar Gaddafi anauawa na waasi.
  • Oktoba 23, 2011: Bendera ya Libya Libya, vita ya wenyewe kwa wenyewe inaisha.

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. Ruthven, Malise (23 June 2016). "How to Understand ISIS". New York Review of Books 63 (11). Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 7 August 2016. Iliwekwa mnamo 12 June 2016.  Check date values in: |date=, |archivedate=, |accessdate= (help)
  2. Fear and Faith in Paradise. Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 28 February 2017. Iliwekwa mnamo October 23, 2014.  Check date values in: |archivedate=, |accessdate= (help)
  3. "Arab Winter". America Staging. Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 26 October 2014. Iliwekwa mnamo October 23, 2014.  Check date values in: |archivedate=, |accessdate= (help)